THE SOWERS GROUP

Friday, June 29, 2012

HALI YA DR ULIMBOKA YAONEANA KUENDELEA VIZURI


WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA KIGENI LA MISAADA WATEKWA NCHINI KENYA

Wafanyakazi wanne wa shirika la kigeni la misaada na mkenya mmoja wametekwa kutoka katika kituo cha wakimbizi kinachoitwa Dadaab kilichpo karibu na mipaka ya somalia. wakati wa sakata hilo dereva aliuawa na mpaka sasa wafanyakazi hao wanne hawajajulika ni wa kutoka taifa gani. hii sio mara ya kwanza kutokea mwaka uliopita matukio kama haya yalijitokeza na kusababisha magrupu mengi ya wafanyakazi hao kuondoka katika kituo hicho kinachosemekana kuwa ni kituo kikubwa cha wakimbizi duniani its more about music industry and social issues in and out of bongo land

Wednesday, June 27, 2012

HIVI ULISIKIA ILE STORI YA WACHEZAJI WA TWIGA STARS KUSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA? KIPYA NDIO HIKI…PA

.

Vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania likiwemo gazeti la Mwananchi vimenukuliwa vikiripoti stori kwamba Kocha wa timu ya taifa ya Twiga Stars aliejiuzulu Boniface Mkwasa alisema moja kati ya mambo yaliyomkera Twiga Stars ni wachezaji kadhaa kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wao kwa wao kwenye timu.

Exclusive on millardayo.com Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili amesema “nimefurahi kulizungumzia hilo swala kwa sababu limekua likizungumzwa kwenye magazeti mengi bila uthibitisho, kocha hakuzungumza kwamba kuna vitendo kama hivyo alisema vilikuepo kipindi cha nyumba lakini kwa sasa havipo, nimekua Twiga Stars toka 2006 mpaka sasa sijaviona hivyo vitendo labda mwalimu ndio aliona kwa mchezaji lakini hakuna yeyote ambae amewahi kuripoti kwangu”

“Wazazi wetu hawajapenda hili swala, tumedhalilishwa na hata kama kuna mchezaji alifukuzwa kutokana na hilo basi itakua ni siri kati yake na mwalimu hatujawahi kuambiwa, kama Mkwasa atapatikana ni vizuri amtaje huyo mtu il iwatanzania wajue lakini kiukweli hakuna vitendo kama hivyo Twiga Stars” – Sophia

Exclusive on millardayo.com leo Kocha Boniface Mkwasa amesema “sijafanya kikao chochote na waandishi wa habari kuzungumzia hilo swala na sijazungumza lolote kuhusu ishu ya usagaji nashangaa hawa waandishi wameipata wapi hii habari na wanazidi kujenga chuki, ndio maana nimekaa kimya wiki nzima sijaongea chochote, na sio kwamba nimetoka Twiga Stars ndio nikasema hayo, sijawahi kushuhudia hivyo vitu hata siku moja na kama vilikuwepo labda ni zamani sana kipindi bado hata sijaingia”

Kuhusu kuvipeleka Mahakamani vyombo vya habari vilivyoandika hizo habari, Mkwasa amesema “mimi sitafanya chochote namwachia Mwenyenzi Mungu tu kwa sababu kila mtu ana uhuru, ila waandishi wazitumie vizuri kalamu zao kwa sababu watasababisha wazazi wasiruhusu mabinti zao kuja kucheza kwenye timu ya taifa”
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...